Nasikia wanadai kulikuwa redline,
Nasikia kuwadai, kwani kuna maisha zina deadline?
Nasikia walicome mtu hamsini, wengine walivuka borderline.
Nasikia huzuni moyoni, walituangamiza ni kama life si divine.
Gova wakaruka wakadai nI siasa.
Wasiasa wakairukia ni ka mchezo wa kudaka.
Wakenya tumekataa, hatutaki tena hu ufala.
Sababu ya ulofa wamelala Kwa kazi, yote wameikwara.
Mi sitafyata na maze masiz na mabro wanago.
Mi sitafyata nikiona wanajaribu kutugawanya.
Mi sitafyata Nikicheki hii hate yote.
Mi sitafyata country yangu ikisahau tulikotoka.
Jameni tuwe wajanja, hivyo tu ndivyo tutaokoka.
Shida zetu hatutazitoroka, pamoja tutaungana kuwashinda.
Ama kweli mnashida, enyi nyi waoga maharamia.
Kunyemelea wasiojihami, waoga nyie katu hamtatushinda.
Haki iwe ngao na mlinzi , tuishi katika uhuru na undugu
Haki iwe ngao na mlinzi , kuisema na kuitenda.
Haki iwe ngao na mlinzi, viongozi kutuendeleza.
Haki iwe ngao na mlinzi, kila siku tuwe na amani.
@elvizbrian.